Wednesday, January 25, 2012

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA MKOANI TANGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya bahari eneo la Pangani Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo.

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji, lililopo wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya mkoa wa Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa & (kushoto) ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, Mohamed Hamis.