Tuesday, April 10, 2012

Taswira Mbalimbali Za Safari ya Mwisho ya Steven Kanumba

Jeneza lenye mwili wa marehemu Kanumba likiwa limebebwa.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Steven Kanumba likiwasili kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.

Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Steven Kanumba asubuhi hii kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam; akifuatiwa na mkewe, pamoja na mke wa Rais,Mama Salma Kikwete (mwenye nguo nyeupe kulia).

Mwili wa marehemu Kanumba ukiwa mbele ya maelfu ya watu kwa ajili ya kuagwa rasmi.

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi 'Sugu' akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa marehemu Kanumba.