Wednesday, January 25, 2012

SOKO LA KISASA LA MWANJELWA JIJINI MBEYA KUENDELEA KUWA KITENDAWILI


Soko jipya la Mwanjelwa lililoanza kujengwa Februari 25,2010 ujenzi wa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2012 ambapo ujenzi huo ulipaswa kukamilika Agosti 24,2011.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Iddi alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali na waandishi wa habari .
Mkurugenzi huyo amesema kuwa soko hilo likikamilika liatarajia kuondoa mlundikano wa wafanyabiashara katika masoko ya Sido na Soweto ambapo tangu juzi wafanyabiashara wa masoko hayo waligoma wakilalamikia kupanda kwa ushuru kwa zaidi ya asilimia 50.