Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Dkt Ali Mohamed Shein amewapongeza wakulima wa zao la karafuu Zanzibar kwa kuweza kuliuzia Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) karafuu kuliko ilivyotarajiwa kwa msimu huu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar;Said Ali Mbaruok akizungumza na Balozi mdogo wa China aliyeko Zanzibar Bibi Sheen Limun (mwenye fulana nyeusi) kuhusiana na maswala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikakati ya kuisadia Zanzibar.